Sunday, August 20, 2017
   
Text Size

Site Search powered by Ajax

image image image image
Chinese journalists visit MCT A delegation of Chinese journalists visited the Media Council of Tanzania (MCT) and exchanged views on how to further cement the cooperation between Chinese and Tanzanian journalists.
MCT launches reports on state of media and investigation on Clouds TV The Media Council of Tanzania (MCT) has formally launched its annual flagship publication – The State of Media for 2016 and a Probe Report on the Invasion of Clouds Media Group.
MCT to launch State of Media Report 2016 and Probe Report on invasion of Clouds TV The Media Council of Tanzania (MCT) will on Monday August 14, 2017 launch its flagship publication – the State of Media Report for 2016 and Probe Report on the invasion of Clouds TV Studios.
Tanzania Daima ordered to apologise to Ludewa DC Tanzania Daima newspaper has been ordered to apologise to the Ludewa District Commissioner, Andrea T’sere for publishing false report about him and his family.

ZA KISWAHILI

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4

Resource Centre

IRC1

Press Clippings

Media Council of Tanzania Website

KESI ya kuipinga sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari namba 12 ya 2016, iliyofunguliwa Januari 18, 2016, katika Mahakama Kuu ya Mwanza, ikipinga baadhi ya vipengele vya sheria kwamba vinakwenda kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeahirishwa hadi Machi 14, 2017.

 Akiahirisha kesi hiyo Jaji Joaquin de Mello, alisema anaahirisha kesi hiyo ili kupata muda wa kupitia maamuzi ya kesi nyingine inayofanana na hii ambayo maamuzi yake yalitolewa Mahakama Kuu Dar es Salaam, ili kujiridhisha kama kuna maeneo yanashabihiana aweze kutoa uamuzi ambao hautakinzana

 Walalamikaji katika Kesi hiyo yenye namba 2/2017, ni Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited.

 Kesi hiyo ilikuwa itolewe maamuzi kama kuna kesi ya kikatiba au la Machi 9, 2017, mbele ya Jaji Mello.

 Wakati huo huo, kesi iliyofunguliwa Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) kuipinga sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari namba 12 ya 2016, imewekewa pingamizi la awali na Serikali.

 Kesi hiyo ilifunguliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wakilalamikia sheria hiyo kwenda kinyume na Mkataba wa Afrika Mashariki.

 Walalamikaji wanatakiwa kujibu pingamizi la serikali ndani ya siku 45 tangu pingamizi hizo lilipowasilishwa Mahakamani hapo.

 Timu ya wanasheria Fulgence Massawe, Edwin Hans, Jenerali Ulimwengu, Jebra Kambole na Mpale Mpoki, inayoziwakilisha taasisi hizo katika Mahakama Kuu, imeanza kuandaa majibu ya pingamizi la Serikali. Mwisho.

 

Media Headlines

MCT Videos
videoMore Videos...

Photo Gallery
photoMore Photos...

Journalism Awards

awaa

Visitors Counter

2145164
Today
All days
728
2145164

OUR RSS

  • No feeds found!